Care Connect Washington ni programu iliyoundwa mapema wakati wa janga ili kupeana chakula na msaada mwingine kwa watu walioambukizwa COVID-19 ili waweze kujitenga nyumbani. Sasa programu hiyo inasaidia kutimiza mahitaji ya muda mrefu ya watu ambao wameambukizwa COVID-19. Kwa mfano, watu wengine hupitia madhara ya muda mrefu ya COVID-19. Watu wengine huenda walikuwa wagonjwa na wakapoteza kazi yao na wanahitaji usaidizi wa kuweza kujitegemea tena. Care Connect Washington inaweza kusaidia.
Care Connect Washington ni ushirikiano kati ya Department of Health (Idara ya Afya), vituo vinane vya ukanda, na zaidi ya waratibu 100 wa ndani katika jamii kwenye jimbo zima. Mfumo wa Care Connect huwezesha jamii kwa kuwasaidia watu kufanikisha uthabiti na afya bora. Waratibu wa utunzaji wa ndani hufanya kazi na mtu ili kuwasaidia kutuma ombi la programu kama vile manufaa ya ukosefu wa ajira, nyumba iliyopungzwa bei au utunzaji wa mtoto, programu za usaidizi wa chakula kama vile Supplemental Nutrition Assistance Program (SNAP, Programu ya Usaidizi wa Lishe ya Ziada) au Special Supplemental Nutrition Program for Women, Infants and Children (WIC, Programu Maalum ya Lishe ya Ziada ya Wanawake, Watoto Wachanga, na Watoto), Apple Health, na zaidi. Care Connect inatoa maelezo ambayo watu wanahitaji katika lugha wanayopendelea.
Mtazamo wa Kiukanda wa Msaada wa COVID-19
Department of Health katika jimbo, ikifanya kazi na mipaka ya afya na washirika wao, inaendesha Care Connect Washington kulingana na kigezo cha eneo hadi eneo. Kila eneo hufanya kazi na washirika wa jumuiya kuwaunganisha watu na huduma wanazostahiki kupata, kama vile uwasilishaji wa matibabu, utunzaji wa kiafya, usaidizi wa kutuma ombi la ukosefu wa ajira, mashirika ya nyumba ya ndani, benki za chakula, watoaji huduma ya utunzaji wa watoto na zaidi.
Huduma Zinapatikana Wapi?
Huduma zinapatikana katika sehemu zote za jimbo kwa watu walioathiriwa na COVID-19.
Ukanda wa Mashariki
Better Health Together (Kiingereza pekee) inahudumu kama Care Connect Washington Kituo cha kaunti za Adams, Ferry, Lincoln, Pend Oreille, Spokane, na Stevens.
Kaunti ya King
HealthierHere (katika Kiingereza pekee) inahudumu kama Kituo cha Care Connect Washington katika Kng County.
Ukanda wa Kaskazini mwa Kati
Action Health Partners katika Kiingereza pekee) inahudumu kama Kituo cha Care Connect Washington katika kaunti za Chelan, Douglas, Grant, na Okanogan.
Ukanda wa Kaskazini
North Sound Accountable Community of Health (katika Kiingereza pekee) inahudumu kama Kituo cha Care Connect Washington katika kaunti za Island, San Juan, Skagit, Snohomish, na Whatcom.
Ukanda wa Kaskazini Magharibi
WithinReach (katika Kiingereza pekee) hutoa huduma za uratibu wa utunzaji katika kaunti za Clallam, Jefferson, na Kitsap.
Kaunti ya Pierce
Elevate Health (katika Kiingereza pekee) inahudumu kama Kituo cha Care Connect Washington katika Pierce County.
Ukanda wa Kusini mwa Kati
Greater Health Now (katika Kiingereza pekee) inahudumu kama Kituo cha Care Connect Washington katika kaunti za Kittitas, Walla Walla, Whitman, Columbia, Garfield, Asotin, Yakima, Benton na Franklin.
Ukanda wa Kusini Magharibi
Southwest Washington Accountable Community of Health (SWACH) (katika Kiingereza pekee) inahumu kama Kituo cha Care Connect Washington katika kaunti Clark, Klickitat, na Skamania.
Ukanda wa Magharibi
Community CarePort (katika Kiingereza pekee) ya Cascade Pacific Action Alliance inahudumu kama Kituo cha Care Connect Washington katika kaunti za Cowlitz, Wahkiakum, Pacific, Grays Harbor, Mason, Thurston, na Lewis.
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara
- Je, huduma Care Connect Washington zinapatikana kwa ajili yangu?
-
Unastahiki kupata huduma iwapo umeambukizwa COVID-19. Hiyo inajumuisha watu ambao kwa sasa ni wagonjwa wanaugua COVID-19 au walikuwa na COVID-19 katika siku zilizopita.
Piga simu kwa 1-833-453-0336. Usaidizi wa lugha unapatikana.
Mratibu wako wa ndani wa utunzaji atawasiliana na wewe ili kufahamu mahitaji yako na kukusaidia kuunganisha na rasilimali na huduma.
- Naweza kutarajia aina gani ya usaidizi?
-
Mratibu wako wa utunzaji wa ndani atachukua muda akipata kukujua na kufahamu mahitaji yako. Kisha watatambua rasilimali za ndani zinazopatikana ili kukusaidia, ikiwa pamoja na utunzaji wa afya, nyumba au utunzaji mtoto uliofidiwa, manufaa ya kukosa ajira, usaidizi wa chakula, na zaidi. Huduma zitatofautiana kulingana na ukanda. Care Connect Washington itatoa maelezo ambayo unahitaji katika lugha unayopendelea. Huduma za Care Connect zinapatikana bila gharama yoyote.
- Itachukua muda upi kabla ya kuweza kupokea usaidizi?
-
Mratibu wako wa utunzaji katika ukanda atafanya kila juhudi kutoa usaidizi ndani ya simu moja baada ya kupokea kutumwa kwako.
- Utalindaje maelezo yangu?
-
Mratibu wako wa utunzaji atathibitisha maelezo wanayopata kutoka kwa kituo cha simu na kuuliza kuhusu mahitaji yako. Maelezo yoyote unayoshiriki na mratibu wako wa utunzaji utasalia kuwa ya siri. Wafanyakazi wanaotoa huduma za uratibu na Department of Health (Idara ya Afya) watatumia maelezo ili kubainisha huduma muhimu ambazo huenda ukahitaji. Hawatashiriki maelezo ya kiafya ya kibinafsi au ya faragha.
- Itanigharimu pesa ngapi?
-
Hutatoza ili kupokea huduma hii. Care Connect Washington ilipokea fedha serikali ya shirikisho za kusaidia katika kukabiliana na COVID-19 katika jimbo la Washington.
- Itachukua muda upi kabla ya kuweza kupokea usaidizi?
-
Mratibu wako wa utunzaji katika ukanda atafanya kila juhudi kutoa usaidizi ndani ya simu moja baada ya kupokea kutumwa kwako.
- Je, bado nitahitaji kujitenga au kukaa katika karantini huku nikipokea usaidizi huu?
-
Ndiyo. Kujitenga na kukaa karantini ni zana muhimu zinazotumika kuepuka kusambaza COVID-19 kwa majirani, marafiki, familia na wafanyakazi wenzi - na kupunguza athari zake hasi zinazowafikia wengi katika jamii zetu. Iwapo unahitaji usaidizi baada ya kipindi chako cha kujitenga au karantini, mratibu wako wa utunzaji katika kanda anaweza kukuunganisha na huduma za ndani za muda mrefu ili kusaidia mahitaji ya kiafya na kijamii yanayoendelea.
- Kuna tofauti gani kati ya kujitenga na karantini?
-
Kujitenga: Ukipatikana na maambukizo ya COVID-19, una dalili, au unasubiri matokeo ya kipimo, unahitaji kujitenga ili kuepuka kusambazia wengine magonjwa yako.
- Kaa nyumbani na kuepuka kugusana na wengine, wakiwemo wanakaya yako.
- Kaa katika chumba tofauti na utumie bafu tofauti, iwapo inawezekana.
- Vaa barakoa inayokutoshea vizuri (katika Kiingereza pekee) iwapo kuna hali ambapo ni lazima uwe karibu na wengine.
- Usiende kazini, shuleni, au katika maeneo ya umma. Epuka kutumia usafiri wa umma, kusafiri pamoja na wengine, au kutumia teksi.
- Kaa nyumbani isipokuwa ikiwa unahitaji huduma ya matibabu.
- Fuata mwongozo wa hivi karibuni zaidi (katika Kiingereza pekee) kutoka kwa Centers for Disease Control and Prevention (CDC ,Vituo vya Udhibiti na Uzuiaji wa Magonjwa (katika Kiingereza pekee) na Department of Health (DOH, Idara ya Afya) (katika Kiingereza pekee) kuhusu urefu wa kipindi cha kujitenga.
Karantini: Iwapo ulikuwa na mfiduo wa COVID-19 lakini huna dalili, unaweza kuhitaji kukaa karantini, kutegemea na hali yako ya chanjo. Hii itazuia kusambaza virusi kabla ya kujua kuwa wewe ni mgonjwa.
Fuata mwongozo wa hivi karibuni zaidi (katika Kiingereza pekee) kutoka kwa CDC (katika Kiingereza pekee) na DOH (katika Kiingereza pekee) kuhusu urefu wa kipindi cha karantini.
- Nafaa kufanya nini iwapo dalili zangu za COVID-19 zitaendelea kuwa hatari?
-
Pata usaidizi wa matibabu kwa haraka ikiwa dalili zako zitaongezeka sana. Iwapo mtu ataonyesha dalili yoyote kati ya zifuatazo, tafuta usaidizi wa kimatibabu wa dharura mara moja:
- Tatizo la kupumua
- Maumivu au shinikizo la muda mrefu kwenye kifua
- Kuchanganyikiwa mpya
- Kutoweza kuamka au kukaa macho
- Midomo au uso wa samawati
*Hii si orodha kamili. Tafadhali wasiliana na mtoa huduma wako wa matibabu kwa dalili nyingine zozote ambazo ni mbaya au zikunatia wasiwasi.
Ukiwa na dharura ya matibabu na unahitaji kupiga 911, mwambie mhudumu huyo kuwa una au huenda una COVID-19. Ikiwezekana, vaa barakoa kabla ya huduma za kimatibabu za dharura kutokea.
- Je, naweza kupokea huduma za Care Connect Washington kwa muda gani?
-
Mratibu wako wa utunzaji katika ukanda atakusaidia kwa hadi siku 21. Katika hali fulani, mratibu wako wa utunzaji anaweza kukuunganisha na huduma za muda mrefu ili kusaidia mahitaji ya kiafya na kijamii yanayoendelea.
- Je, Care Connect Washington inafanya kazi vipi?
-
Care Connect Washington ni mtazamo unaoauniwa na jimbo, unaojikita sana maeneo ya ndani kwa utunzaji unaoratibiwa.
Washington State Department of Health inasimamia juhudi za uratibu wa utunzaji katika ukanda, inasaidia kuajiri na kutoa mafunzo, inazuia mapengo katika rasilimali za jimbo zima na za ndani, na kuhakikisha matokeo ya juu zaidi kwa kusimamia rasilimali zilizokusanywa pamoja, kama vile ufadhili na muundomsingi wa kiufundi.
Kanda maalum hutambua na kutuma jopo kazi linalojikita katika jamii ili kutoa usaidizi na kuunganisha watu kwa rasilimali za ndani ili kusaidia kujitenga na kukaa karantini kwa mafanikio. Kanda hizo zinafanya kazi na wauzaji wa ndani ili kusambaza bidhaa na huduma zinazohitajika, kusaidia kuchangia kwa ufufuaji wa uchumi wa ndani.
Waratibu wa utunzaji wametolewa ili kutathmini, kusaidia, na kufuatilia afya na mahitaji ya kijamii ya kipekee ya kila mtu na kuunda Mpango wa Hatua ya Utunzaji wa COVID. Mpango huo unaunganisha watu na rasilimali katika lugha wanayopendelea popote panapowezekana na kuwaelekeza kwenye mchakato wa kuhakikisha kuwa wamesaidiwa.
- Utalindaje maelezo yangu?
-
Mratibu wako wa utunzaji atathibitisha maelezo wanayopata kutoka kwa Nambari ya Simu ya Taarifa ya COVID-19 na kuuliza kuhusu mahitaji yako. Maelezo yoyote unayoshiriki na mratibu wako wa utunzaji utasalia kuwa ya siri. Wafanyakazi wanaotoa huduma za uratibu na Department of Health watatumia maelezo ili kubainisha huduma muhimu ambazo huenda ukahitaji. Hawatashiriki maelezo ya kiafya ya kibinafsi au ya faragha.
- Care Connect Washington huzuia vipi msambao wa COVID-19?
-
Watu wanaopokea usaidizi wa kukidhi mahitaji ya kijamii na kiafya wana uwezekano mkubwa zaidi wa kufanikiwa kukamilisha kujitenga nyumbani na kukaa kwenye karantini. Kwa kuhakikisha kuwa watu ambao wamepatikana na maambukizo ya COVID-19 au walikuwa na mfiduo kwa mtu mwingine aliyeambukizwa huendelea kujitenga au kukaa karantini, Care Connect Washington inaweza kupunguza msambao wa COVID-19 na kuboresha ufufuaji wa uchumi. Kwa sababu mfumo uawalenga watu walio na mahitaji ya kiafya na kijamii ambao wanaweza kudhurika zaidi na COVID-19, inaweza kusaidia kutatua ukosefu uliopo wa usawa kiafya na kusaidia jamii zilizoathiriwa na COVID-19.
- Nawasiliana na nani iwapo namjua mtu ambaye anahitaji utunzaji kutoka kwa Care Connect Washington?
-
Iwapo wewe au mtu unayemjua amejitenga kwa uamilifu au ameingia karantini nyumbani na anahitaji usaidizi, wasiliana na Nambari ya Simu ya Taarifa ya COVID-19 ya Jimbo.
Nambari ya Simu ya Taarifa ya COVID-19 ya Jimbo: Bofya 1-800-525-0127, kisha ubonyeze #. Usaidizi wa lugha unapatikana.
- Jumatatu saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku
- Saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni, Jumnne hadi Jumapili, na sikukuu za jimbo zinazofuatiliwa
- Je, Care Connect Washington inajumuisha huduma za afya ya kitabia?
-
Ndiyo! Mratibu wako wa utunzaji anaweza kukusaidia kupata huduma za kiafya za kitabia katika jamii yako.
- Je, huduma za msaada wa uratibu wa usaidizi zina[atikana kwa wanachama wa Tribal Nations (Mataifa ya Kikabila)?
-
Ndiyo. Ili kujifunza zaidi, tuma barua pepe kwa COVID19.CareCoordination@doh.wa.gov aupiga 564-999-1565.
- Je, huduma za ukalimani zinapatikana?
-
Ndiyo. Ukipiga Nambari ya Simu ya Maelezo ya COVID-19 katika 1-800-525-0127 na kisha kubonyeza #, usaidizi wa lugha utapatikana.
Mara tu umeunganishwa kwa mratibu wa utunzaji, Care Connect Washington itatoa maelezo ambayo unahitaji katika lugha unayopendelea.
Rasilimali
- Ukurasa wa Wavuti wa Rasilimali na Mapendekezo Pata taarifa zaidi kuhusu nguo za kufunika uso, karantini, kutoa huduma ya utunzaji kwa familia, mfiduo wa COVID-19, dalili, na zaidi. Unaweza kupanga nyenzo za lugha unayopendelea.